IQNA

Klipu | Tilaawa ya Surah Al-Kawthar kwa Sauti ya Ustadh Ja‘far Fardi

Tehran – Ustadh Ja‘far Fardi, qari mashuhuri wa kimataifa kutoka Iran, usiku wa Ijumaa tarehe 30 Jumada l-Ula , alisoma ya aya tukufu za Qur’ani katika usiku wa kwanza wa maombolezo ya Bibi Fatima Zahra (AS) ndani ya Husseiniyya ya Imam Khomeini (MA) jijini Tehran.

Katika kikao hicho cha maombolezo unyenyekevu, alisoma Surah Al-Kawthar kwa sauti ya kipekee, na kuwakumbusha waumini baraka na rehema za Mwenyezi Mungu kwa Mtume Muhammad (SAW). Kipande cha tilaawa hiyo kimewekwa kwa watazamaji ili kushuhudia ladha ya Qur’ani Tukufu ikisomwa kwa utulivu na unyenyekevu.